Home Uncategorized AZAM FC YAWEKA PEMBENI HISTORIA YA YANGA, YAZITAKA POINTI TATU

AZAM FC YAWEKA PEMBENI HISTORIA YA YANGA, YAZITAKA POINTI TATU


 UONGOZI wa Azam FC umesema kuwa wanaitazama mechi yao ya kesho dhidi ya Yanga kipekee kwa kuweka hali ya hofu pembeni zaidi. 


Kocha Msaidizi wa Azam FC, Bahati Vivier amesema kuwa wapo tayari kwa ajili ya mchezo wa kesho kwa namna yoyote kutokana na maandalizi ambayo wameyafanya.

“Ukitazama mechi ya kesho tunacheza na Yanga ni timu kubwa iyenye historia la hiyo historia tunaiweka pembeni na tuna imani tutafanya vizuri.


“Mechi yetu dhidi ya KMC hali haikuwa nzuri na hatukuwa na mchezo mzuri lakini kwa namna ambavyo tumejipanga tuna amini tutafanya vizuri.


“Tutakuwa nyumbani na tutaingia uwanjani kusaka pointi tatu na kupata ushindi kwenye mchezo wetu muhimu,” amesema.


Mshindi wa kesho anajenga nafasi ya kuwa kinara huku ikiwa itapitikana sare basi Yanga itabaki nafasi ya pili kwa kuwa imefunga mabao machache tofauti na Azam FC.


Azam FC ipo nafasi ya kwanza baada ya kufunga mabao 18 huku Yanga ikiwa nafasi ya pili baada ya kufunga mabao 13.


Zote zikiwa zimecheza mechi 11, zimekusanya pointi 25 kibindoni.


Azam FC imepoteza michezo miwili ilikuwa mbele ya Mtibwa Sugar kwa kufungwa bao 1-0 na ule wa hivi karibuni dhidi ya KMC kwa kufungwa bao 1-0 Novemba 21.


Inakutana na Yanga ambayo haijafungwa mchezo hata mmoja kwa msimu wa 2020/21 hivyo kazi itakuwa kubwa ndani ya Uwanja wa Azam Complex.

SOMA NA HII  KIKOSI CHA MTIBWA SUGAR LEO DHIDI YA SIMBA UWANJA WA JAMHURI, MOROGORO