Home Uncategorized ABDI BANDA: TUNAPIGA MATIZI KAMA KAWAIDA

ABDI BANDA: TUNAPIGA MATIZI KAMA KAWAIDA

ABDI Banda nyota wa Tanzania anayekipiga ndani ya Klabu ya Highlands Park inayoshiriki Ligi Kuu Afrika Kusini amesema kuwa wanapiga matizi kama kawaida ili kulinda vipaji vyao lakini ni ndani ya nyumba.

Kwa sasa Ligi ya Afrika Kusini na nyingine nyingi duniani zimesimamishwa ili kupisha maambukizi ya Virusi vya Corona.

“Tunapiga mazoezi huku kwa sasa licha ya kwamba hali sio shwari kwani Corona imetufanya tushinde ndani tukifanya mazoezi ambayo tumepewa na makocha wetu.

“Pia wanafuatilia maendeleo yetu ili kujua ni namna gani tunakuwa bora kwa kuwa kazi ya mchezaji ni lazima acheze na kulinda kipaji pia kupitia mazoezi ni muhimu,” amesema.

SOMA NA HII  MUONEKANO WA UKURASA WA MBELE GAZETI LA CHAMPIONI IJUMAA