Home Uncategorized FEI TOTO: NINACHUKUA TAHADHARI YA CORONA NA KUFANYA MAZOEZI

FEI TOTO: NINACHUKUA TAHADHARI YA CORONA NA KUFANYA MAZOEZI


KIUNGO Mkabaji wa timu ya Yanga, Feisal Salum, ‘Fei Toto’ amesema kuwa kwa sasa anaendelea kufanya mazoezi ili kuwa bora na anachukua tahadhari ya kujilinda na Virusi vya Corona.

Kwa sasa Ligi Kuu Bara imesimama kupisha maambukizi ya Virusi vya Corona.

Fei Toto amesema:” Kuna vingi ambavyo tunavikosa lakini ni muhimu kujali na kufikiria afya zetu kwani ni muhimu kuliko kitu kingne kwanza.

“Nafanya mazoezi ili kuwa bora na ninachukua tahadhari kuhusu Corona imani yangu hali itakuwa poa na tukirudi nitakuwa kwenye ubora,” amesema.

SOMA NA HII  MUONEKANO WA UKURASA WA MBELE GAZETI LA SPOTIXTRA ALHAMISI