Home Uncategorized MORATA: KUMKABILI DIJK NI HABARI NYINGINE

MORATA: KUMKABILI DIJK NI HABARI NYINGINE


ALVARO Morata, mshambuliaji wa Klabu ya Atletico Madrid amesema kuwa kukabiliana na beki kitasa wa Liverpool, Virgil van Dijk kunahitaji akili kwani ni ngumu mithili ya kupanda mlima.

Mshambuliaji huyo amesema kuwa kupenya kwenye himaya ya beki huyo ni jambo la kujivunia kutokana na umakini wake.



Nyota huyo mwenye miaka 27 alikuwa kwenye kikosi kilichoshinda mabao 4-2 dhidi ya Liverpool ambao ulikuwa ni wa Ligi ya Mabingwa Ulaya.


Amewataja mabeki wengine visiki kukabiliana nao ambao ni Sergio Ramos wa Real Madrid na Giorgio Chiellini wa Juventus.


Staa huyo yupo kwa mkopo ndani ya Atletico Madrid akitokea Chelsea ambapo amecheza jumla ya mechi 38 na kutupia mabao 14.

SOMA NA HII  NYOTA SIMBA KUIBUKIA POLISI TANZANIA, ATOA MASHARTI MAGUMU