Home Uncategorized RONALDINHO NA KAKA YAKE WAPATA DHAMANA

RONALDINHO NA KAKA YAKE WAPATA DHAMANA


HATIMAYE Ronaldinho nyota wa zamani wa Klabu ya Barcelona na timu ya Taifa ya Brazil na kaka yake Assis wamepata dhamana na kutoka gerezani nchini Paraguay baada ya kukaa huko kwa siku 32.

Ronaldinho na Kaka yake wamepata dhamana kwa dola milioni 1.6 (Tsh Bilioni 3.7) baada ya awali kukataliwa dhamana nyepesi kwa hofu wangeweza kutoroka.

Pamoja na kupata dhamana hiyo jaji Gustavo Amarilla ameamuru wawili hao kutolewa gerezani na kwenda kuishi katika nyumba/hotel katika mji wa Asuncion wakiwa chini ya uangalizi maalum.

Ronaldinho na Assis walikamatwa na Polisi nchini Paraguay kwa tuhuma za kuingia nchini humo na Passport feki za Paraguay ambazo zinawaonesha wao kama raia wa nchi hiyo wakati ni raia wa Brazil.
SOMA NA HII  YANGA YAINDIA ANGA ZA MTUPIAJI HUYU MZAWA