Home Uncategorized SIMBA YATOA TAMKO KUHUSU KUFUTWA KWA LIGI KUU BARA

SIMBA YATOA TAMKO KUHUSU KUFUTWA KWA LIGI KUU BARA


OFISA Mtendaji Mkuu wa Simba (C.E.O), Senzo Mazingisa, amesema kuwa ni mapema sana kufanya mgawanyiko juu ya ligi ifutwe ama iendelee kwani bado wanasubiri maamuzi ya Serikali na Bodi ya Ligi.
Ligi Kuu Bara imesimama kwa sasa kupisha agizo la Serikali la kusimamisha shughuli zote za michezo nchini ili kuepusha maambukizi ya Virusi vya Corona.
Senzo amesema kuwa itakuwa mapema kwao kutoa maoni ya ligi kufutwa ama kuendelea kwani wanasubiri maamuzi ya Serikali na Bodi ya Ligi juu ya ligi hiyo.
“Serikali ilitoa siku 30 ambazo hazijamalizika bado, lakini pia Bodi ya Ligi wana maamuzi yao na sekta nyingine zinazosimamia michezo hapa nchini, hivyo tumewaachia na sisi tutafuata yanayotakiwa kufuatwa.
“Japo malengo yetu yalikuwa ni kuhakikisha tunachukua ubingwa wa ligi kuu msimu huu ili tushiriki michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika msimu ujao ikiwa ni sehemu ya malengo yetu tuliyojiwekea,” amesema kiongozi huyo.
Simba inaongoza ligi ikiwa na pointi 71, ikiwa na nafasi kubwa ya kutwaa ubingwa msimu huu, kwani Azam wanawafuatia wakiwa na pointi 54, hivyo kama likija suala la kufutwa kwa ligi, itakuwa ni hasara zaidi kwa Simba.

Chanzo: Championi
SOMA NA HII  SIMBA QUEENS WASHUSHA WINGA MPYA KUTOKA CONGO