Home Uncategorized DANNY ROSE YEYE NI MWENDO WA MKOPO TU MWANZO MWISHO

DANNY ROSE YEYE NI MWENDO WA MKOPO TU MWANZO MWISHO


DANNY Rose, beki wa Klabu Tottenham Hotspur amecheza jumla ya mechi 156 ndani ya klabu hiyo na ametupia mabao nane huku maisha yake yakiwa ni mwendo wa mkopo tu.

Kwa sasa anakipiga ndani ya Klabu ya Newcastle United kwa mkopo ambapo alijiunga nayo mwaka 2020.

Aliibukia ndani ya klabu hiyo akitokea Sunderland ambapo napo alikuwa kwa mkopo na alicheza mechi 27 na kufunga bao moja ilikuwa ni msimu wa 2012/13.

Pia hata alipojiunga na Sunderland alitoka kukipiga Bristol City msimu wa 2010/2011 kwa mkopo alitua hapo akitokea Paterborough United msimu wa 2009 napo alikuwa kwa mkopo akitokea Klabu ya Watford ambapo alicheza kwa mkopo pia.

SOMA NA HII  DIARRA KAMA KAWA DHIDI YA AL AHLY