Home Uncategorized FIFA YAIBONYEZEA CHEKUNDU TUZO YA MCHEZAJI BORA 2020 MAZIMA

FIFA YAIBONYEZEA CHEKUNDU TUZO YA MCHEZAJI BORA 2020 MAZIMA

SHIRIKISHO la Soka la Kimataifa (Fifa) limetangaza kufuta tuzo za soka zinazotolewa na Shirikisho hilo mwaka huu kutokana na janga la Virusi vya Corona. 
Tuzo hizo zilitarajiwa kutolewa jijini Milan nchini Italia, Septemba 2020.

Washindani wawili duniani ambao ni Lionel Messi anayekipiga Barcelona na Cristiano Ronaldo ambao ni washindani wakubwa hawatakuwa na cha kubeba mwaka huu Kwenye kipengele cha Mchezaji Bora wa Mwaka.

Gianni Infantino, Rais wa Fifa amekuwa akiweka wazi msimamo wake kuwa wanachukua tahadhari kubwa dhidi ya janga la Virusi vya Corona. 

Kuhusu tuzo za Ballon d’Or ambazo zimekuwa zikitolewa kila mwaka tangu 1956 haijulikani hatma yake mpaka sasa.

SOMA NA HII  HIKI NDICHO ANACHOKIFANYA MORRISON KUJILINDA NA CORONA