Home Uncategorized HAWA JAMAA KWA SARE NDO MPANGO KAZI WAO, ADOLF NDO KUBWA LAO

HAWA JAMAA KWA SARE NDO MPANGO KAZI WAO, ADOLF NDO KUBWA LAO


KWENYE Ligi Kuu Bara kabla haijasimamishwa kutokana na janga la Virusi vya Corona ushindani ulikuwa ni mkali mwanzo mwisho.

Kuna baadhi ya timu ilikuwa ni mgumu kusepa na pointi tatu wakikubali ni sare ya namna yoyote ile.

 Wababe ni Tanzania Prisons iliyo chini ya Kocha Mkuu Adolf Rishard ikiwa imecheza mechi 30 imejikusanyia pointi 14 kati ya 41 ilizonazo kwa sasa kwa kulazimisha sare 14.
 

Biashara United imejikusanyia pointi 10 kati ya pointi 40 ilizonazo kwa kulazimisha sare 10 baada ya kucheza mechi 29.

Mwadui FC imejikusanyia pointi 10 kati ya 34 ilizonazo kwa kulazimisha sare 10 Kwenye mechi 28.

Ndanda FC imesepa na pointi 10 kati ya 31ilizonazo baada ya kucheza mechi 29 ikiwa na pointi 31 kibindoni.


Yanga imesepa na pointi 9 ikiwa imecheza mechi 27 kati ya pointi 51 ilizonazo kibindoni imelazimisha sare 9.

Mbeya City kati ya pointi 30 ilizonazo, 9 ilisepa nazo kwa sare baada ya kucheza mechi 29.

7. JKT Tanzania ina sare 9 ikisepa na pointi 9 kati ya 42 zilizopo kibindoni baada ya kucheza mechi 28.

SOMA NA HII  MTUPIAJI MWINGINE TENA ANASWA KMC