Home Uncategorized ISHU YA MWAMNYETO KUMALIZANA NA YANGA IPO HIVI

ISHU YA MWAMNYETO KUMALIZANA NA YANGA IPO HIVI


NAHODHA na beki wa kati wa Coastal Union, Bakari Mwamnyeto amekiri kuwepo kwenye mazungumzo mazuri ya kukamilisha dili lake la kusaini mkataba wa miaka miwili ya kukipiga Yanga.
Beki huyo ni kati ya wachezaji waliokuwepo kwenye mazungumzo ya kukamilisha usajili wake wa kutua Yanga katika kuboresha safu ya ulinzi ya timu hiyo inayochezwa hivi sasa na Mghana, Lamine Moro, Kelvin Yondani, Andrew Vincent ‘Dante’ na Juma Makapu.

Staa huyo wa Coastal hivi karibuni alikuwa anatajwa kwenye usajili wa Simba kuelekea msimu ujao kabla ya Yanga chini ya wadhamini wao GSM kuingilia kati dili hilo la usajili.
Mwamnyeto amesema kuwa Yanga wapo kwenye hatua za mwisho na mabosi wa klabu hiyo kukamilisha usajili wake wa kutua Jangwani.

Mwamnyeto amekiri kufuatwa na baadhi ya klabu za ndani na nje ya nchi zilizomfuata ambazo wameshindwana katika maslahi huku akiitaja Yanga ndiyo iliyokuwepo katika hatua za mwisho za kukamilisha dili hilo la usajili.
Aliongeza kuwa kikubwa kilichompeleka Yanga ni maslahi mazuri na siyo kitu kingine ambapo yeye mwenyewe amekubaliana na hivi karibuni atasaini mkataba wa awali.
“Nipo kwenye mazungumzo mazuri na Yanga, kikubwa ninachokiangalia hivi sasa ni maslahi pekee yatakayonifanya nisaini mkataba wa kuichezea Yanga katika msimu ujao.
“Zilikuwepo klabu nyingi zilizokuwa kwenye mipango ya kuwania saini yangu lakini nimeshindwana nazo katika maslahi na siyo kingine, lakini Yanga yenyewe imeonyesha nia nzuri ya mimi kujiunga nayo.
“Ninafahamu Yanga upo ushindani mkubwa wa namba, lakini hiyo hainifanyi niogope kujiunga na Yanga, nimejiandaa kwa ajili ya kupambana na siku zote mimi siogopi ushindani,” amesema Mwamnyeto.

Chanzo:Championi 
SOMA NA HII  YANGA NA MIPANGO YA POINTI TATU ZA AL AHLY