Home Uncategorized MAMBO BADO SIO SHWARI LAKINI LAZIMA KUJIPANGA NA KUCHUKUA TAHADHARI DHIDI YA...

MAMBO BADO SIO SHWARI LAKINI LAZIMA KUJIPANGA NA KUCHUKUA TAHADHARI DHIDI YA CORONA


MAPAMBANO bado yanaendelea kwa sasa kwani kila mmoja anazidi kutafuta njia ya kuona namna gani anaweza kutoka pale alipo,

Mengi ambayo tunayasikia hasa kutoka kwenye vyombo husika kuhusu maambukizi ya Virusi vya Corona hatupaswi kupuuzia hata kidogo kwani ni kwa faida za afya zetu.
Tunaona kwamba Serikali imeweza kuona namna gani watu wake ambavyo wamekosa mpira kwa muda mrefu kutokana na janga la Corona ambalo linaitesa dunia.
Kwa kuwa tayari Rais, John Pombe Magufuli amesema kuwa kuna mpango wa kufikiria namna gani anaweza kuruhusu ligi kurejea kuna umuhimu wa kuangalia namna gani tutajiaandaa kurejea kwenye ligi.
Kitu cha msingi ni kuishukuru Serikali kwa kujali na kutazama namna mambo yanavyokwenda hasa kwenye ligi za Tanzania ambazo zilikuwa zimesimama kwa muda.
Imani yangu ni kwamba maandalizi yanaweza kuanza kwa Shirikisho la Soka Tanzania kuangalia namna gani wanaweza kuanza kujiaandaa kwa ajili ya kumaliza msimu huu wa 2019/20
Hatua makini zinapaswa zianze kuandaliwa kwa sasa kwa kuwa ni muda mrefu ligi zilikuwa zimesimama na hakukuwa na mambo yanayoendelea kwenye soka na mipango mingi ilikuwa kimya kutokana na Corona.
Kauli ya Serikali iwashtue pia wachezaji ambao walikuwa wameacha kabisa kufanya mazoezi ama walikuwa wakifanya kwa kutegea jambo ambalo sio zuri kwa afya zao.
Ikiwa wataedelea na tabia zao za kutofanya mazoezi wakati wa kuonyesha kile walichokuwa wakikifanya unakuja kwani ni suala la muda tu kurejea kwa ligi nchini Tanzania.
Ligi Daraja la Kwanza, Ligi Daraja la Pili, Ligi ya Wanawake na zile za mkoa pia hazikuwa kwenye mwendelezo kwani mambo mengi yalisimama na kwa sasa ni muda wa kuzinduka kuanza kujipanga upya.
Ngumu kusema kwamba lini itarejea lini kwani Serikali inatambua kwamba licha ya kuwa ni muhimu ligi kuendelea na afya za wachezaji pamoja na raia wake ni muhimu pia.
Wakati sahihi ni kuanza kujipanga muda huu kwa kila mmoja ili pale ligi itakaporejea mambo yawe sawa na kusiwe na sababu nyingine ambazo zitawafanya wachezaji ama viongozi wa timu kushindwa kuendelesha timu zao.
Iwapo kila timu itakuwa kwenye maandalizi mazuri italeta ushindani ambao ulikuwa umeanza kushika kasi ila ulisitishwa kutokana na janga la Corona ambalo linaitikisa dunia.
Pia mwendelezo wa kuchukua tahadhari kwa kila mmoja na mwanafamilia ya michezo ni jambo la kuzingatia ili kuendelea kuwa salama kwani afya ni kitu cha msingi.
Wizara ya afya imekuwa ikitoa mrejesho na taarifa mara kwa mara kuhusu namna ya kujilinda na kuchukua tahadhari ni muhimu kufuata utaratibu unaotolewa na Serikali.
Yapo masuala ya kila mmoja kuvaa barakoa na kwa wale ambao wanaingia kwenye ofisi kupata huduma ni muhimu kufuata taratibu hizo ili kuwa salama zaidi.
Kikubwa kitakachotuvusha salama hapa ni kufuata utaratibu uliowekwa na kuwa makini kwenye kujali afya zetu ambazo ni mtaji mkubwa wa kwanza.
Ugonjwa huu upo na unaitikisa dunia tusijisahau kwa kuendelea kuishi maisha yale ambayo tuliyazoea zamani ni muda wa kubadilika na kuongeza umakini zaidi.
Ni muhimu kufuata maelekezo ya Serikali na kufuata kanuni za afya ili kujilinda sisi wenyewe hii vita tumeanza ni lazima tuimalize kwa ushindi inawezekana.
Asiwepo wa kubaki nyuma katika hili kwani dunia ni lazima tuungane na tufanye kazi kwa kushirikiana ili kushinda kwani ushindi wa mtu mmoja ni mwanzo wa kufungua ushindi kwa taifa.
Tunaona kwa sasa watoto wapo nyumbani wakiendelea kusubiri tamko la Serikali kurudi shule kuendelea na masomo nao pia wanapaswa wafuate kanuni.
Ulinzi wa mtoto unapaswa uwe mkubwa ili pale atakaporejea shule awe na afya ya kutosha na uwezo wa kuendelea kupambania ndoto zake.
Pia ni wakati wa timu zote Bongo kuungana katika vita hii ili kutengeneza dunia yao nyingine kwa kuacha ule uhasama ambao wanakuwa nao hasa wanapokutana uwanjani.
Manahodha wa timu na viongozi ni wakati wa kuunganisha nguvu na kuwa kitu kimoja kwani ni muhimu kuunganisha nguvu kushinda hii vita ambayo tumeianza.
Ni muhimu kutambua kwamba dunia inapambana kwa wakati huu kutafuta matokea sahihi lakini tusijisahau kwa kufanya yale ambayo hayajaelekezwa na wataalamu wetu kwa wakati huu wa kupambana na Corona.
Basi kwa wakati huu ni sahihi kuungana pamoja kuanza kazi upya ya kuongeza nguvu kupambana na Virusi vya Corona kwa vitendo na itakuwa rahisi kwetu kushinda.
Zipo timu ambazo zimeanza kufanya kazi kwa vitendo kupambana na Virusi vya Corona na kuna makampuni mengine ambayo yanaendelea kupambana na Corona kwa vitendo.
Ni vema kutambua kwamba uhitaji ni mkubwa kwa wakati huu hivyo kwa wale ambao wanauwezo ni muhimu kujitoa na kuungana kusaidia wale wahitaji.
Kwa wale ambao wameanza kupambana kwa vitendo ninawapa pongezi na kuwapa moyo kwamba wasichoke kufanya hivyo kazi hiyo ni njema na ina mataokeo hapo baadaye.
Kwa kuanza kwao iwe ni mwanzo kwa wengine kuendelea kujitoa kusaidia jamii na kupambana na Corona kwa vitendo kwani muda bado upon a mahitaji pia yapo kila siku.
Tusijisahau na kufikiri kwamba mambo yatakuwa mepesi ilihali hakuna ambaye anachukua tahadhari kwani afya ni utajiri kwa kila mmoja.
Bado nafasi ipo kwa sasa haina maana kwamba ni lazima iwe kwa makundi hapana dunia imebadilika na teknolojia imekuwa kubwa.
Wachezaji, timu na mashabiki pamoja na makampuni ni muda wa kuendelea kutoa sapoti kwa vitendo kupambana na adui huyu ambaye anapoteza furaha ya wengi duniani.
Napenda kuwakumbusha na wachezaji kwamba wasisahau kuendelea kutimiza zile program ambazo walipewa na benchi la ufundi iytasaidia kuwarejesha kwenye ubora wao.
Kuishia kufanya mazoezi kwa kutegea kunarudisha nyuma maendeleo ya timu pamoja na wanafamilia ya michezo kiujumla hivyo rai wangu kila mmoja kutimiza majukumu yake.
Viongozi, TFF, wachezaji na timu ni muda wa kujiaadaa vema kwa ajili ya ligi kurejea ili kushinda changamoto ambazo zitatokea hapo baadaye.
SOMA NA HII  ISHU YA MAKAME KUIKANA YANGA IPO HIVI