Home Uncategorized MTUPIAJI WA MBAO FC ANA OFA NNE MKONONI

MTUPIAJI WA MBAO FC ANA OFA NNE MKONONI


WAZIR Jr, mtupiaji namba moja wa Klabu ya Mbao FC amesema kuwa ana ofa nne mkononi kwa sasa anasubiri wakati ufike afanye maamuzi.
Wazir amehusika kwenye mabao 9 kati ya 19 yaliyofungwa na Mbao FC msimu huu ambapo ametupia kimiani saba na kutoa pasi mbili za mabao.
Nyota huyo amesema kuwa mkataba wake ndani ya Mbao FC unamalizika msimu utakapomeguka huku akiwa na ofa mkononi zaidi ya nne.
“Nina ofa nyingi kutoka timu mbalimbali ambazo zinahitaji saini yangu ikiwa ni pamoja na mabosi wangu wa sasa ambao ni Mbao FC wenyewe.
“Timu nyingine siwezi kuziweka wazi kwa sasa kwa kuwa wakati bado haujafika ila ni nyingi zaidi ya nne wakati ukifika nitajua nitakuwa wapi,” amesema Wazir.

Kwa sasa Ligi Kuu Bara imesimama kutokana na janga la Virusi vya Corona ambavyo vimeivuruga dunia. 
SOMA NA HII  NGASSA AJICHIMBIA MWANZA KWA SASA