Home Uncategorized AJIBU AMERUDI,AFUNGA BAO LA KIDEO SIMBA IKISHINDA MABAO 3-1 MBELE YA KMC

AJIBU AMERUDI,AFUNGA BAO LA KIDEO SIMBA IKISHINDA MABAO 3-1 MBELE YA KMC


IBRAHIM Ajibu, kiungo mshambuliaji wa Simba leo amefunga bao la kideo dakika za usiku wakati Simba ikiifunga mabao 3-1 KMC kwenye mchezo wa kirafiki uliochezwa Uwanja wa Simba Mo Arena uliopo Bunju.

KMC ilikuwa ya kwanza kuandika bao la kuongoza dakika ya 30 kupitia kwa mshambuliaji wake Charles Ilanfya bao hilo lilisawazishwa na John Bocco dakika ya 34 na bao la pili akafunga dakika ya 75 na Ajibu alifunga bao la tatu dakika ya 88.

Huu unakuwa ni mchezo wa pili wa kirafiki Simba kucheza leo ambapo mechi ya kwanza walicheza asubuhi na Transit Camp na kushinda mabao 4-2.

KMC wameendeleza utamaduni wao wa kucheza soka safi la pasi za kuonana  pamoja na kutengeneza nafasi nyingi ambazo  walikuwa wakipoteza wanapofika ndani ya 18.

SOMA NA HII  MUONEKANO WA UKURASA WA MBELE GAZETI LA CHAMPIONI JUMAMOSI