Home Uncategorized CHAMA NI MWENDO WA MATIZI TU, AKOSA MECHI MBILI BONGO

CHAMA NI MWENDO WA MATIZI TU, AKOSA MECHI MBILI BONGO

KIUNGO Mshambuliaji wa Simba, Clatous Chama jana alianza mazoezi yake rasmi kujiweka fiti kwa ajili ya kuweza kuungana na wenzake kwenye kikosi.

Chama alianza kufanya mazoezi peke yake akiwa chini ya Kocha wa viungo, Adel Zraine ambaye amekuwa akimsimamia ili kumrejesha kwenye ubora wake.

Chama alikosa mechi zote mbili za kirafiki ambazo Simba ilicheza kwa kuwa bado hajawa fiti kuungana na wenzake kwenye mechi za ushindani.

Simba ilicheza mechi mbili ambapo ya kwanza ilikuwa dhidi ya Trsansit Camp ambapo ilishinda mabao 4-2 na mechi ya pili ilishinda mabao 3-1 dhidi ya KMC kwenye Uwanja wa Mo Simba Arena uliopo Bunju.

Chama alitua Jumatatu akitokea nchini Zambia ambapo alikuwa huko baada ya Serikali kusitisha masuala ya michezo kutokana na janga la Virusi vya Corona kwa sasa Serikali imeruhusu masuala ya michezo kuendelea kwa kueleza kuwa hali ya maambukizi imepungua.

SOMA NA HII  TANZIA:KATIBU BASATA ATANGULIA MBELE ZA HAKI