Home Uncategorized DAVID LUIZ KUONGEZEWA DILI LA MWAKA MMOJA

DAVID LUIZ KUONGEZEWA DILI LA MWAKA MMOJA


DAVID Luiz, nyota anayekipiga ndani ya Arsenal amekubali kuongeza saini ya mwaka mmoja kuendelea kuitumikia timu hiyo iliyo chini ya Kocha Mkuu, Mikel Arteta.

Beki huyo wa kati amekuwa akishushiwa lawama kutokana na kuwa chanzo cha kichapo cha mabao 3-0 mbele ya Manchester City, Juni 17,2020 alitolewa nje kwa kuonyeshwa kadi nyekundu dakika ya 49.

Kwa makosa aliyofanya, Luiz aliomba msamaha na wengi wakiamini kuwa itakuwa mwisho wa kubaki ndani ya kikosi hicho kwa kuwa mkataba wake unameguka Juni 30.

Mpaka jana, Jumanne, inaelezwa uongozi wa Arsenal ulikuwa kwenye mpango wa kuzungumza naye huku wakihitaji kubaki naye mpaka mwaka 2021.

SOMA NA HII  MO AZUIA TENA PRESS YA HAJI MANARA SIMBA