JADON Sancho, ameungana na dunia kiujumla kutetea haki ya George Floyd ambaye inaripotiwa kuwa aliuawa na Polisi mweupe wa Marekani kwa sababu za kiubaguzi wa rangi kwa kuwa yeye ni mweusi, mjini Minneapolis.
Jana, Mei 31, Sancho alifunga hat trick take ya kwanza ndani ya Borussia Dortmund, wakati wakiinyoosha mabao 6-1 Padernborn kwenye mchezo wa Bundesliga. Muda wa kushangilia mshambulijaji huyo alionyesha fulana yenye maneno ya kuhitaji kuona haki ya Floyd inapatikana.
Sancho alipachika mabao hayo dakika ya 57,74 na 90+2 huku mengine yalifungwa na Thorgan Hazard dakika ya 54, Achraf Hakimi ambaye ni beki dakika ya 85 naye aliungana na Sancho kwa kuonyesha t shirt yenye ujumbe sawa na Sancho, Marcel Schmelzer dakika ya 89 alipachika bao huku lile la Paderborn likipachikwa kwa penalti na Uwe Hunembeier dakika ya 72.
Ushindi huo unaifanya Dortmund kufikisha pointi 60 ikiwa nafasi ya pili ikiachwa kwa pointi 7 na vinara ambao ni Bayern Munich wenye pointi 67 huku Paderborn ikiwa nafasi ya 18 na pointi zake 19 zote zimecheza mechi 29.