Home Uncategorized JEMBE LA KAZI YANGA, MORRISON LAANZA MATIZI LEO

JEMBE LA KAZI YANGA, MORRISON LAANZA MATIZI LEO


BERNARD Morrison kiungo mshambuliaji wa Yanga leo amejiunga na wachezaji wenzake kwenye mazoezi yanayofanyika Uwanja wa Chuo cha Sheria,Sinza, Dar es Salaam.

Morrison hakuwa sehemu ya kikosi kwa wachezaji waliosafiri kwenda Shinyanga na Dodoma ambapo alikosa mechi mbili za Ligi Kuu Bara kwa kile kilichoelezwa kuwa alikuwa na matatizo yake binafsi.


Mechi ambazo alizikosa ni pamoja na ile dhidi ya Mwadui FC iliyochezwa Uwanja wa Kambarage Juni 13 na Yanga ilishinda bao 1-0 pamoja na mchezo dhidi ya JKT Tanzania uliochezwa Juni 17 Uwanja wa Jamhuri, Dodoma na Yanga ililazimisha sare ya kufungana bao 1-1.

Yanga imeanza mazoezi leo ikiwa ni maandalizi ya mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Azam FC utakaochezwa Juni 21, Uwanja wa Taifa.

Kocha Mkuu wa Yanga, Luc Eymael amesema kuwa ana imani Morrison ataendelea kutimiza wajibu wake ndani ya Yanga.

SOMA NA HII  MIMBA YA MPENZI WA DIAMOND YAWA GUMZO