Home Uncategorized KISA KUGAWANA POINTI MOJA NA RUVU, SIMBA WATOA TAMKO HILI

KISA KUGAWANA POINTI MOJA NA RUVU, SIMBA WATOA TAMKO HILI


UONGOZI wa Simba umesema kuwa sare ya kufungana bao 1-1 na Ruvu Shooting Uwanja wa Taifa leo sio aina ya matokeo mazuri ambayo waliyatarajia.

Simba imekubali kusepa na pointi moja mbele ya Ruvu Shooting kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara uliokuwa na ushindani mkubwa.

Simba ilianza kupata bao kupitia kwa Shiza Kichuya dakika ya 11 ambalo lilisawazishwa na Fully Maganga dakika ya 39.

Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara amesema kuwa:”Ni matokeo ambayo tumeyapata sio mazuri kwani hatukutarajia kupata matokeo haya hasa kwa Simba ila mwisho wa siku ulikuwa ni mchezo mzuri lazima tukubali matokeo.

Ofisa Habari wa Ruvu Shooting, Masau Bwire amesema:”Wachezaji wetu wamepambana na hili nilisema tangu jana kwamba haitakuwa kazi nyepesi, umepigwa ule mpira wenyewe wa pale Barcelona hivyo bado moto wetu unaendelea.”

SOMA NA HII  KAMA KAWAIDA YAKE, MANARA AKIWASHA KWA KOCHA MPYA YANGA, AWAVAA MASHABIKI - VIDEO