Home Uncategorized KOCHA AYAKATAA MABAO YA BOCCO WA SIMBA

KOCHA AYAKATAA MABAO YA BOCCO WA SIMBA

KOCHA Mkuu wa KMC, Harerimana Haruna amesema kuwa kichapo cha mabao 3-1 walichopata kutoka kwa Simba sio halali kwa kuwa mabao mawili yaliyofungwa na nahodha John Bocco alikuwa ameotea.

Simba iliwafunga KMC kwenye mchezo wa kirafiki uliochezwa Juni 8, Uwanja wa Simba, Mo Arena.

Mabao ya Simba mawili yalifungwa na Bocco huku moja likifungwa na kiungo mshambuliaji wa Simba, Ibarahim Ajibu.

“Tumefungwa bao moja la halali hivyo matokeo yaliyo sahihi ni 1-1, mabao mawili ya Bocco yote aliotea hivyo mimi sijui imekuajekuaje,” amesema.

Bao la KMC lilipachikwa kimiani na Charlse Ilanfya ambaye alikuwa ni mwiba ndani ya Simba.

SOMA NA HII  JUVENTUS WAMUOMBA RONALDO ASISEPE