Home Uncategorized MBEYA CITY YAGOMA KUSHUKA DARAJA

MBEYA CITY YAGOMA KUSHUKA DARAJA

AMRI Said, Kocha Mkuu wa Mbeya City amesema kuwa wachezaji wake wapo tayari kwa ajili ya mapambano ya ligi kwa mechi ambazo zimebaki.

Mbeya City imebakiwa na mechi tisa ili kukamilisha mzunguko wa pili wa ligi huku wakiwa kwenye hatari ya kushuka daraja iwapo watashindwa kuchanga karata zao vizuri.

Said amesema:”Tunatambua tunachokitaka ndani ya ligi, mechi zetu ambazo zimebaki tutapambana kupata matokeo chanya ili tubaki kwenye ligi msimu ujao kwani wachezaji wapo tayari na morali ni kubwa,” amesema.

Ikiwa imecheza mechi 29 kibindoni imejikusanyia pointi 30 ikiwa nafasi ya 17.

SOMA NA HII  MBUNGI YA AZAM vs YANGA KUPIGWA SIKU HII WIKI IJAYO