Home Uncategorized MNIGERIA : HUYU NDEMLA HUYU..!!!

MNIGERIA : HUYU NDEMLA HUYU..!!!

STRAIKA wa Mwadui FC, Raphael Aloba ‘Obina’ amesema kupotezwa na viungo wa Simba SC, wakiongozwa na Said Ndemla ndio sababu iliyowafanya kukumbana na kipigo cha mabao 3-0 katika mchezo huo wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Obina mwenye mabao sita Ligi Kuu Bara, alisema Simba walikuwa na nguvu kubwa katika eneo la kiungo ambalo mbali na Ndemla walikuwa wakicheza Mbrazil, Gerson Fraga, Hassan Dilunga na Luis Miquissone.

Mnigeria huyo, alisema, “Ndemla alikuwa bora katika mchezo wa Jumamosi, aliifanya Simba itawale eneo lote la kiungo, nadhani walituzidi hapo tukawa tunatumia nguvu kubwa kushambulia, ilitubidi washambuliaji tuwe tunashuka chini kusaidia.”

“Ukiangalia hata ile mechi dhidi ya Yanga nao walituzidi katika eneo la kiungo, nadhani mwalimu atafanyia kazi upungufu mwingine ambao ameuona ili tumalize vizuri msimu.”

Baada ya mchezo huo wa Jumamosi kocha wa Simba SC, Sven Vandenbroeck alipoulizwa kuhusu kiwango cha Ndemla alisema sababu ya kumuanzisha katika mechi hiyo ni kutokana na kujituma kwake mazoezini wakati wakijiandaa na mchezo huo hivyo mchezaji yeyote ana nafasi ya kuanza katika kikosi chake cha kwanza.

SOMA NA HII  SIMBA YATAJA SABABU ITAKAYOWAPA UBINGWA MSIMU WA 2020/21