Home Uncategorized BIASHARA UNITED KUANZA NA UONGOZI

BIASHARA UNITED KUANZA NA UONGOZI

UONGOZI wa Biashara United umesema kuwa kwa sasa unajipanga kufanya uchaguzi ili kupata viongzoi wapya ndani ya timu hiyo.

Katibu wa Biashara United, Haji Mtete amesema kuwa hesabu kubwa kwa sasa ni kuona wanafanikisha lengo la kupata viongozi wapya watakaoongoza timu hiyo kwa muda wa miaka minne.

“Uchaguzi unatarajiwa kufanyika mwezi Agosti 7 mwaka huu kwa lengo la kupata viongozi wapya, nafasi ambazo zitafanyiwa uchaguzi ni pamoja na Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti na nafasi ya wajumbe wanne,” amesema.

SOMA NA HII  GLOBAL FC KUMALIZANA NA DSJ FC MAZIMA LEO