Home Uncategorized SIMBA YATAJA SABABU ITAKAYOWAPA UBINGWA MSIMU WA 2020/21

SIMBA YATAJA SABABU ITAKAYOWAPA UBINGWA MSIMU WA 2020/21

 


UONGOZI wa Simba umesema kuwa unazidi kujiweka sawa kwa ajili ya kutetea taji lao la Ligi Kuu Bara walilotwaa msimu wa 2019/20 kwa sababu wana kikosi imara na chenye wachezaji wazuri wenye ushirikiano.


Tayari imecheza mechi tano kwa msimu wa 2020/21, imekusanya pointi 13 baada ya kushinda mechi nne na kulazimisha sare ya kufungana bao 1-1 na Mtibwa Sugar,  Uwanja wa Jamhuri, Morogoro. 


Meneja wa Simba, Patrick Rweyemamu amesema kuwa mpango mkubwa wa timu hiyo ni kuweza kutwaa tena ubingwa kwa msimu wa 2020/21.


“Tuna mechi nyingi na ngumu hasa ukizingatia kwamba ligi ina ushindani mkubwa hilo lipo wazi ila malengo yetu ni kuona kwamba tunashinda mechi zetu na kupata matokeo mazuri.


“Sababu kubwa ya sisi kufanya hivyo ni kuwa na kikosi kizuri ambacho kinapata matokeo kwa kadri ambavyo kinahitaji, mbinu na ushirikiano ndani ya Simba ni vitu vinavyotupa mafanikio,” amesema. 

Ikiwa imecheza jumla ya mechi tano na kufunga mabao 14 kinara wao wa utupiaji ni Meddie Kagere mwenye mabao manne. 

SOMA NA HII  KOCHA STARS:TUTAPAMBANA KUPATA MATOKEO DHIDI YA BURUNDI