Home Uncategorized MTAMBO WA MABAO NDANI YA TANZANIA PRISONS, KESHO MBELE YA SIMBA ITAKUWA...

MTAMBO WA MABAO NDANI YA TANZANIA PRISONS, KESHO MBELE YA SIMBA ITAKUWA BALAA SOKOINE


TANZANIA Prisons ina vipaji kibao vyenye uwezo mkubwa na spidi ndani ya Uwanja katika kutafuta matokeo kwa namna yoyote.

Ikiwa chini ya Kocha Mkuu, Adolf Rishard, falsafa yake kubwa ni kuambulia angalau pointi hata moja kwa mpinzani hapo mbinu yake itakuwa imetimia. 

Ikiwa imecheza jumla ya mechi 31 za Ligi Kuu Bara kibindoni ina pointi 15 ilizobeba kwa kuambulia sare 15 na mchezo wake wa mwisho mbele ya JKT Tanzania alilazimisha sare ya kufungana mabao 2-2 Uwanja wa Sokoine. 

Kesho, Uwanja wa Sokoine anakutana na Simba iliyo chini ya Kocha Mkuu, Sven Vandenbroec ambaye kwa upande wa beki wa pembeni anamtegemea Shomari Kapombe kumwaga maji.

Kwa Prisons yupo kijana mzawa asiye na makuu uwanjani, anaitwa Salum Kimenya, mtambo wa mabao ndani ya kosi hilo la wajelajela.

Jezi yake mgongoni anayoipenda kuivaa  ni namba 14 akiwa ndani ya Uwanja ni kiraka na itategemea nafasi gani Kocha Mkuu, Adolf Rishard atampanga.

Mbali ya kuwa ni beki akiwa amecheza mechi 24 kati ya 31 ambazo Prisons imecheza anatupia nyavuni na anatengeneza nafasi za mabao.

Kibindoni ana mabao manne aliyoyajaza kimiani na ametengeneza mabao manne ya kufunga kwa wachezaji wenzake anaitwa Kimenya kama Kimenya.

Kazi yake nyingine ndani ya uwanja ni kumwaga maji kati kama ilivyo kwa Kapombe wa Simba hapa tofauti yao ni moja tu Kimenya ana ushkaji mkubwa na lango.

Msimu wa 2018/19 alikuwa namba moja kwa mabeki wenye mabao mengi kimiani alijaza mabao saba na kwa sasa ndiye baba lao kwa kucheka na nyavu akiwa na mabao manne.

Kona na faulo zimekabidhiwa miguuni mwake akiwa fiti kama fiti huwa anaonyesha ule ubabe wake, yupo Tanzania Prisons kitambo anaitambua falsafa ya Prisons pamoja na Simba, kesho Uwanja wa Sokoine itakuwa ni balaa zito.

 Simba ikipiga hesabu za kutangazwa kuwa mabingwa, Lrisons inawaza tano bora.

SOMA NA HII  KAGERA SUGAR YAWAITA MASHABIKI KAITABA, YAZITAKA POINTI TATU ZA MWADUI