Home Uncategorized OLE GUNNAR APANGA KUMTUMIA POGBA NA BRUNO

OLE GUNNAR APANGA KUMTUMIA POGBA NA BRUNO


OLE Gunnar Solskjaer, Kocha Mkuu wa Manchester United inaripotiwa kuwa amepanga kumtumia kiungo wake Paul Pogba kucheza namba 10 sambamba na kiungo Bruno Fernandes.

Pogba tayari amesharejea kutoka kutibu majeraha yake ya enka ambayo aliyapata jambo ambalo linampa matumaini makubwa Solsksjaer kuona namna atakavyokuwa na kikosi kipana chenye muunganiko makini.

Tayari Pogba ameanza mazoezi na wachezaji wenzake huku akiwa ni mwenye furaha na aliweza kuonana na kiungo mwenzake Fernades ambaye amekuwa na msaada mkubwa ndani ya kikosi cha United.

Kiungo huyo hajacheza mechi ya ushindani tangu Boxing day mwaka jana kutokana na kutumia muda mwingi kutibu majeraha yake.
SOMA NA HII  KOCHA:KAGERE ATAWAFUNGA SANA KWA MWENDO HUU