Home Uncategorized SAKATA LA MORRISON LIKIWA LIMETUA TFF, SIMBA WALIJIBU KIMTINDO NAMNA ISHU ILIVYO

SAKATA LA MORRISON LIKIWA LIMETUA TFF, SIMBA WALIJIBU KIMTINDO NAMNA ISHU ILIVYO


WAKATI Uongozi wa Klabu ya Yanga ukiwa umepeleka malalamiko Shirikisho la soka nchini (TFF) kuhusu kushawishiwa winga wake Bernard Morrison kujiunga na klabu nyingine kinyume cha sheria,ili haki itendeke wapinzani wao wamejibu kimtindo.

Inaelezwa kuwa Morrison amekuwa akishawishiwa na Simba ili atue ndani ya klabu hiyo jambo ambalo limekuwa likileta mvutano kwa pande zote mbili na hivi karibuni alisema kuwa ameshawishiwa na baadhi ya viongozi ambao walimpa fedha.

Kaimu katibu Mkuu wa Yanga, wakili Simon Patrick amesema klabu haiwezi kufumbia macho maelezo yaliyotolewa na winga huyo ambaye ameweka wazi kila kilichotokea. 


‘Mchezaji wetu ameeleza kila kitu,hivyo tumepeleka malalamiko yetu TFF na chombo husika kitasikiliza kutokana na ushahidi tuliouwasilisha na kutolea maamuzi.


Patrick amesema tayari ushahidi umekusanywa kwa ajili ya suala hilo ikiwa ni pamoja na kumhoji mchezaji na vielelezo vingine vinavyohusiana na suala hilo.

Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara amesema kuwa miongoni mwa klabu ambazo zinatambua kanuni za usajili ni pamoja na Simba hivyo hawahusiki katika masuala ya usajili wa mchezaji huyo.

SOMA NA HII  JUHUDI YA WACHEZAJI YANGA YAMKOSHA KAZE