Home Uncategorized YANGA WAINYOOSHA MABAO 2-0 DAR CITY

YANGA WAINYOOSHA MABAO 2-0 DAR CITY


KLABU ya Yanga leo imeshinda mabao 2-0 kwenye mchezo wa kirafiki dhidi ya Dar City uliochezwa Uwanja wa Chuo cha Sheria.

Mchezo wa kwanza Yanga ilishinda kwa mabao 3-1 dhidi ya Transit Camp ambayo leo usiku itakuwa na kibarua cha kumenyana na Azam FC Uwanja wa Azam Complex.

Kocha Msaidizi wa Yanga, Charles Mkwassa amesema kuwa maandalizi wanayoyafanya ni kwa ajili ya kurejesha wachezaji wake kwenye ubora baada ya kukaa nje kwa muda mrefu.

Mabao ya Yanga yalifungwa na Adeyum Saleh pamoja na Mohamed Issa,’Mo Banka’.

Juni 7 watakuwa na mchezo wa kirafiki dhidi ya KMC utakaochezwa Uwanja wa Uhuru na utakuwa ni mchezo wa mwisho kabla ya kuanza safari kuifuata Mwadui FC, Uwanja wa Kambarage, Shinyanga.

SOMA NA HII  WANYARWANDA WAFUNGUKA USAJILI WA KIFAA KIPYA CHA YANGA..!!