Home Uncategorized BREAKING:WAAMUZI WA YANGA V AZAM FC TAIFA YAWAKUTA, WAFUNGIWA MIEZI MITATU

BREAKING:WAAMUZI WA YANGA V AZAM FC TAIFA YAWAKUTA, WAFUNGIWA MIEZI MITATU




ELLY Sasii mwamuzi wa kati wa mchezo wa Yanga na Azam FC pamoja na wasaidizi wake Sudi Lila na Mbaraka Haule wamefungiwa miezi mitatu kwa kosa la kutokuumudu mchezo huo uliochezwa Juni 21, 2020 katika Uwanja wa Taifa, Jijini Dar es Salaam.

Taarifa iliyotolewa leo kupitia ukurasa rasmi wa Shirikisho la Soka Tanzania wa Instagram imeelza kuwa adhabu hiyo imetolewa kwa uzingativu wa kanuni ya 39(1) kuhusu udhibiti wa waamuzi.


Mechi hiyo ilikamilika kwa sare ya bila kufungana kwa timu zote mbili ambapo ziligawana pointi moja moja.

Mchezo huo ulikuwa ni wa Ligi Kuu Bara ambapo Azam FC waliandika baru Bodi ya Ligi Juni 22 baada ya kutoridhishwa na maamuzi ya waamuzi hao kukataa mabao mawili pamoja na penalti.

SOMA NA HII  MO HAELEWIELEWI INAKUAJEKUAJE NDANI YA SIMBA