Home Uncategorized GUU LA KAGERE LAPATA TABU DAKIKA 208 NDANI YA UWANJA

GUU LA KAGERE LAPATA TABU DAKIKA 208 NDANI YA UWANJA


MACHI 11 Uwanja wa Uhuru, Meddie Kagere alifunga bao dakika ya 71 wakati Simba ikishinda mabao 8-0 mbele ya Singida United kwa pasi ya Hassan Dilunga wakati akifikisha jumla ya mabao 19. Kwenye mchezo huo Kagere alifunga mabao manne na kusepa na mpira wake wa kwanza.
Baada ya hapo Ligi Kuu Bara ilisimamishwa kutokana na janga la Virusi vya Corona na Kagere alisepa zake Rwanda. Juni Mosi Serikali iliruhusu masuala ya michezo kuendelea.
Mpaka inatwaa ubingwa, Simba ilikuwa imecheza mechi tano ambazo ni sawa na dakika 360, huku Kagere akitumia dakika 208 na hajaambulia bao wala kutoa pasi ya bao kwenye mechi alizocheza.

Kwenye mechi dhidi ya Azam FC, alitumia dakika zote kukaa benchi akisoma mchezo na timu yake ilishinda mabao 2-0.

Alianza kucheza mbele ya Ruvu Shooting, Juni 14 aliyeyusha dakika zote 90 kwenye sare ya kufungana bao 1-1 Uwanja wa Taifa kisha mechi yake ya pili ikawa ni Juni 17 Uwanja wa Taifa dhidi ya Mwadui ambapo Simba ilishinda mabao 3-0, Kagere alitumia dakika 28.
Mwisho wa yote guu la kushoto la Kagere lilishindwa kufurukuta mbele ya Tanzania Prisons iliyo chini ya Kocha  Mkuu, Adolf Rishard Uwanja wa Sokoine ambapo aliyeyusha dakika zote 90 na kufanya atumie jumla ya  dakika 208 ndani ya uwanja bila kufurukuta.
Kagere anavutwa shati na mtupiaji namba moja wa Kagera Sugar, mzawa Yusuph Mhilu ambaye kibindoni ana jumla ya mabao 13.
SOMA NA HII  YANGA HII NI JEURI, MILIONI 930 KUSAJILI JEMBE