Home Uncategorized KUMUONA MORRISON AKIFANYA YAKE TAIFA MBELE YA SIMBA BUKU 10 TU

KUMUONA MORRISON AKIFANYA YAKE TAIFA MBELE YA SIMBA BUKU 10 TU

SHIRIKISHO la Soka Tanzania, (TFF) kupitia kwa Bodi ya Ligi imeweka wazi viingilio katika mchezo wa hatua ya nusu fainali ya Kombe la Shirikisho kati ya Simba na Yanga, Uwanja wa Taifa, kesho majira ya saa 11:00 jioni.

Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi Tanzania Almas Kasongo amesema kuwa wamejipanga katika mchezo huo kuingiza mashabiki wasiozidi elfu 30 kutokana na kuchukua tahadhari dhidi ya Virusi vya Corona. 

“Tumejipanga vizuri kuelekea kwenye mchezo wa kesho hasa katika upande wa mashabiki watakaoingia ni 30,000 ikiwa ni nusu ya watu 60,000 na tuna imani suala hilo litazingatiwa hivyo ninaomba watanzania waheshimu hilo.

“Kwa upande wa viingilio, tumeongeza kidogo ili kupunguza watu, 30,000 VIP A, sh. 25,000 VIP B,sh 20,000 kwa C wakati mzunguko ikiwa ni sh.10,000 jambo la msingi ni kukata tiketi mapema katika vituo ambavyo vitawekwa wazi na zitaanza kuuzwa leo,”.

Mchezo huu unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa ambapo Simba wanakumbukumbu ya kufungwa bao 1-0 lililofungwa na Bernard Morrison Uwanja wa Taifa kwa mpira wa faulo uliozama moja kwa moja langoni.

SOMA NA HII  VPL: MTIBWA 0-0 SIMBA