Home Uncategorized SportPesa YAMKABIDHI MSHINDI WA JACKPOT SportPesa MAMILIONI

SportPesa YAMKABIDHI MSHINDI WA JACKPOT SportPesa MAMILIONI


KAMPUNI ya Michezo na Burudani ya SportPesa Tanzania leo imemkabidhi mshindi wa Jackpot SportPesa, Jamal Khalfan Abdallah Shilingi 288, 974, 720 baada ya kuibuka mshindi.
Hii ni awamu ya nne kwa Jackpot ya SportPesa kupata mshindi kutoka wilaya ya Ilala, Dar baada ya washindi wengine watatu kujizolea mamilioni kupitia ubashiri huo wa michezo.
Jamal mwenye umri wa miaka 26 mkazi wa Ilala jijini Dar-es-Salaam, amejishindia kiasi hicho cha pesa baada ya kubashiri mechi 13 za Jackpot kwa usahihi.
Akizungumza leo jijini Dar es Salaam wakati wa kumtangaza mshindi huyo, Mkurugenzi wa Utawala na Udhibiti SportPesa Tanzania Bwana Tarimba Abbas amesema kuwa Bw. Jamal ameshinda Jackpot hiyo baada ya kubashiri mechi 13 zilizochezwa mwishoni mwa wiki kwa usahihi.
“Mpaka sasa SportPesa imeshatoa zaidi ya Sh Bil 1.8 kwa washindi wanne wa jackpot kwa kubashiri kwa usahihi mechi 13. Pia tangu tuanze biashara Mei, 2017 hadi leo hii washindi wa Jackpot na bonasi wamelipwa zaidi ya Bil 8.2.
“Tunafurahi kwa kipindi cha miaka mitatu mfululizo kubadili maisha ya watanzania mbalimbali na kuongeza familia ya mamilionea,” alisema Tarimba na kuongeza kuwa.
“SportPesa ni kampuni inayofuata taratibu zote ili kuhakikisha sheria zilizowekwa na bodi ya michezo ya kubahatisha zinafuatwa ikiwa pamoja na kulipa kodi. Kodi iliyolipwa kwa washindi wote wa Jackpot waliopatikana kuanzia 2017 tumeweza kurudisha kodi kwa Serikali kwa zaidi ya shilingi Bilioni 1.6.
“Nitoe rai kwa watanzania wote na wapenda michezo kuwa SportPesa ipo kwa ajili ya kuwaburidisha hasa kwenye ubashiri wa mipira ya miguu na mara zote mshindi huwekewa pesa zake kwenye akaunti yake papo hapo,” alisema Tarimba.
Akizungumza mara baada ya ushindi wake, Jamal alisema kuwa “Sikutegemea kama nitashinda maana niliweka mikeka zaidi ya kumi, hivyo nilitegemea kupata bonasi na sio Jackpot.
“Hizi pesa nilizoziweka kwa hivi sasa sitazitumia na badala yake nitaziweka kwanza benki kwa muda huku nikifikiria nini cha kufanya, kwa sababu hizi pesa ni nyingi kwani utulivu mkubwa unahitajika.
“Mimi ninajishughulisha na ujasiriamali kwa hivi sasa, hivyo kupitia ushindi wangu huu ninaamini nitafanikisha mahitaji yangu muhimu,”
“Pesa nilizoshinda nimelipa shilingi 57,794,944/- kama kodi kwa Serikali na kiasi kilichobakia ambacho ni zaidi ya Mil 231 nitapunguza pia asilimia 10 na kutoa msaada kwa watoto yatima.
“Nashabikia sana timu ya Young Africans na nimefurahi sana SportPesa kuniletea wachezaji kama sapraizi ya leo na katika pesa hizi za ushindi asilimia kumi nitatoa msaada kwa Watoto Yatima,”alisema Jamal.
SOMA NA HII  KUMBE, CHILUNDA KOCHA ALIMKATAA MOROCCO