Home Uncategorized YANGA YAIFUATA LIPULI, YATOA HESHIMA KWA HAYATI MKAPA

YANGA YAIFUATA LIPULI, YATOA HESHIMA KWA HAYATI MKAPA


TIMU ya Yanga leo imeanza safar kuelekea mkoani Iringa kwa ajili ya kujiaandaa na mchezo wa Ligi Kuu Bara utakaochezwa Julai 26, Uwanja wa Samora dhidi ya Lipuli.

Kikosi cha Yanga kilikuwa Morogoro ambapo kimetoka kumalizana na Mtibwa Sugar kwenye mchezo wa ligi uliochezwa Julai 22 Uwanja wa Jamhuri.

Mchezo huo walitoshana nguvu kwa kufungana bao 1-1 ambazo zimewafanya Yanga wafikieshe pointi 69 kibindoni wakishushwa nafasi ya pili na Azam kwa tofauti ya mabao ya kufunga.

Mchezo huo unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa kwa kuwa Lipuli inahaha kusaka nafasi ya kubaki ndani ya ligi huku Yanga ikihitaji kumaliza ikiwa nafasi ya pili.

Lipuli ipo nafasi ya 13 ikiwa na pointi 44 haina uhakika wa kubaki ndani ya ligi inahitaji pointi tatu ili kujiongezea uhakika wa kubaki.

Kabla ya kuanza safari leo Kikosi kikosi kilisimama kwa dakika moja ili kutoa heshima kufuatia kifo cha Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu,Benjamin William Mkapa.

SOMA NA HII  GEORGE LWANDAMINA AWAPA TANO WACHEZAJI WAKE