Home Uncategorized ATLETICO MADRID, MANCHESTER UNITED ZAINGIA ANGA ZA BARCELONA

ATLETICO MADRID, MANCHESTER UNITED ZAINGIA ANGA ZA BARCELONA



KLABU ya Barcelona ipo kwenye mpango wa kumuuza kiungo wao Ivan Rakitic kwa dau la pauni milioni 17 msimu huu huku Atletio Madrid ikiwa mstari wa mbele kuinasa saini ya nyota huyo.

Kiungo huyo mwenye miaka 32 anapigiwa pia hesabu na Manchester United iliyo chini ya Ole Gunnar Solksjaer ambaye anahitaji kuboresha kikosi chake.

Mkataba wa Rakitic ambaye ni nahodha msaidizi kwenye timu ya Taifa ya Croatia ambayo ilitinga kwenye Fainali za Kombe la Dunia mwaka 2018 ilipoteza mchezo huo mbele ya Ufaransa.

Mkataba wake umebakiza mwaka mmoja ambapo akiwa ndani ya Barcelona amecheza mechi 298 ameshinda mataji  manne ya La Liga mataji manne ya Copa del Rey na Kombe la Ligi ya Mabingwa mwaka 2015.
SOMA NA HII  NYOTA WA MWADUI AIYEE AWAAMBIA YANGA WAPELEKE MKWANJA MREFU