Home Uncategorized AJIBU WA SIMBA ANATAJWA KUIBUKIA KMC

AJIBU WA SIMBA ANATAJWA KUIBUKIA KMC


INAELEZWA kuwa kiungo mshambuliaji wa Simba, Ibrahim Ajibu anaweza kutolewa kwa mkopo kukipiga ndani ya Klabu ya KMC.

Ajibu alijiunga na Simba kwa dili la miaka miwili akitokea Klabu ya Yanga hajawa na nafasi kwenye kikosi cha kwanza kilicho chini ya Sven Vandenbroeck.

 Akiwa Yanga kwa msimu wa 2018/19 ametoa jumla ya pasi 17 na alikuwa kinara ila msimu huu ndani ya Simba ametoa pasi tano.

Kinara wa kutoa pasi ndani ya Simba msimu huu ni Clatous Chama ambaye ametoa pasi 10 za mabao. 

Mtendaji Mkuu wa Simba, Senzo Mazingisa amesema kuwa suala la wachezaji watakaochwa itawekwa wazi. 

SOMA NA HII  HIVI NDIVYO BAO LA MORRISON LILIVYOTINGA BUNGENI