Home Uncategorized KOCHA MRUNDI AANZA KAZI RASMI YANGA

KOCHA MRUNDI AANZA KAZI RASMI YANGA

 ALIYEWAHI kuwa kipa wa Azam FC, Vladimir Niyonkuru raia wa Burundi aliwasili rasmi nchini Tanzania, juzi mchana tayari kwa kuanza kazi ya kuwanoa makipa wa Yanga kuelekea msimu ujao wa 2020/21.

 

Yanga ambayo kwa sasa ipo katika mkakati wa kujijenga upya kufuatia kufumua benchi lake lote la ufundi baada ya msimu wa 2019/20 kufikia tamati, ilimuondoa aliyekuwa kocha wake, Luc Eymael raia wa Ubelgiji baada ya kutoa lugha ya kibaguzi.


Tayari leo Agosti 28 imemtangaza  kocha mpya atakayebeba mikoba ya Eymael ambaye ni Zlatico Krmpotick aliyekuwa akikinoa kikosi cha Polokwane City kwa kandarasi ya miaka miwili.


 Kocha huyo aliwasili juzi na kisha jana Alhamisi alianza kazi kwa kutoa maelekezo katika mazoezi ya timu yake hiyo mpya.

 

Yanga ilifanya mazoezi kwenye Uwanja wa Chuo cha Sheria, Ubungo jijini Dar, na kocha huyo alikuwa bize kuwanoa makipa wa timu yake.


“Tumeshafanikiwa kumpata kocha wa makipa Niyonkuru raia wa Burundi ameshaanza kazi,” amesema mtoa taarifa huyo.

SOMA NA HII  BAKARI MWAMNYETO: MAMBO YAKIWA FRESH, NINASAINI YANGA