Home Uncategorized MASHABIKI YANGA WAOMBWA KUSAJILI WACHEZAJI WAWILI WA KIMATAIFA

MASHABIKI YANGA WAOMBWA KUSAJILI WACHEZAJI WAWILI WA KIMATAIFA

 


UONGOZI wa Yanga umesema kuwa una wachezaji wawili wazuri wa kimataifa ambao tayari umeshazungumza nao ila unapenda kurejesha usajili wao mikononi mwa mashabiki ili waweze kuwasijili wachezaji hao.


Mwenyekiti wa Yanga, Mshindo Msolla amesema kuwa wana imani na mashabiki na wadau wa timu hiyo hasa katika masuala ya kujitolea kwa ajili ya timu yao hivyo wanaamini watafanikisha bila matatizo.

“Tunawachezaji wa kimataifa wawili ambao tayari tumeshazungumza nao kila kitu, ila tunaomba hawa gharama za usajili zifanywe na mashabiki na wadau ambao wamekuwa nasi kila wakati.


“Uwezo ninajua upo kwa sababu msimu uliopita walisajili wachezaji 10 mashabiki wenyewe ila msimu huu tunaomba waweze kusajili wachezaji wawili tu na utaratibu utatolewa hivi karibuni,” amesema.

SOMA NA HII  KIUNGO MUANGOLA RASMI ATUA BONGO KUMALIZANA NA YANGA