Home Uncategorized MASHINE MPYA ZA SIMBA ZAMPA WAKATI MGUMU SVEN

MASHINE MPYA ZA SIMBA ZAMPA WAKATI MGUMU SVEN

 


KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck amesema ana wakati mgumu wa kuwapanga wachezaji wake katika nafasi ya ushambuliaji kutokana na kuwa wengi huku wote wakiwa na uwezo mkubwa.

 

Sven raia wa Ubelgiji, ameongeza kuwa ujio wa wachezaji wapya akiwemo Chriss Mugalu na Bernard Morrison, umezidi kumpa wakati mgumu zaidi.Safu ya ushambuliaji ya Simba kwa msimu ujao itakuwa na Mugalu, Morrison, Meddie Kagere, John Bocco na Charles Ilanfya.


Kocha huyo amesema: “Nina mastraika wanne kwa sasa ambao wote ni wazoefu, mechi moja inataka wawili, hiyo ina maana wawili watakaa benchi lakini pia wanaweza wasiwepo kabisa kwa sababu kuna wachezaji wa nafasi nyingine nao wanataka kucheza.


“Kila mmoja anaonyesha uwezo wake kwenye mazoezi kulishawishi benchi la ufundi ili kupata nafasi ya kucheza, hili ni jambo zuri kwa kocha kwa sababu nina nafasi kubwa ya kuchagua na kujaribu mifumo mingi zaidi katika kikosi changu.


“Kikubwa ambacho nitakuwa nikitazama ni namna ya kuwa na kikosi chenye ushindani kwani nina amini kila atakayeanza ataonyesha kitu cha kipekee zaidi,” amesema.

SOMA NA HII  ISHU YA CHAMA KUIBUKIA YANGA, UONGOZI WA SIMBA WAJIBU NAMNA HII