Home Uncategorized PIRLO ARITHI MIKOBA YA SARRI KWA MIAKA MIWILI JUVENTUS

PIRLO ARITHI MIKOBA YA SARRI KWA MIAKA MIWILI JUVENTUS

MCHEZAJI wa zamani wa Juventus, Andrea Pirlo ameteuliwa kuwa kocha wa timu hiyo, saa chache baada ya Maurizio Sarri kutimuliwa. 

Pirlo mwenye miaka  41, amesaini mkataba wa miaka miwili ambao utadumu mpaka mwaka 2022 akichukua mikoba ya Sarri aliyetimuliwa baada ya timu yake kushindwa kutinga hatua ya robo fainali Ligi ya Mabingwa Ulaya. 

 

Kiungo huyo wa zamani wa Italia siku 9 zilizopita alipewa jukumu la kuwa kocha wa timu ya vijana chini ya miaka 23 kwenye klabu hiyo lakini hivi sasa Pirlo amethibitishwa rasmi kama mrithi wa mikoba ya Sarri.

 

Akiwa na Juventus ameshinda ubingwa wa Kombe la Dunia 2006 akiwa na Italy, Bingwa wa Serie A mara sita, baada ya kushinda mbili na Milan na mara nne akiwa na Juve. Alishinda ndoo mbili za Ligi ya Mabingwa akiwa na Milan, 2003 na 2007. Bingwa wa Coppa Italia mbili na Italia Super Cup.

SOMA NA HII  MUONEKANO WA UKURASA WA MBELE GAZETI LA SPOTI XTRA ALHAMISI