Home Uncategorized SANCHO MAMBO NDANI YA MANCHESTER UNITED MAMBO YANAZIDI KUPAMBA MOTO

SANCHO MAMBO NDANI YA MANCHESTER UNITED MAMBO YANAZIDI KUPAMBA MOTO


JADON Sancho ameripotiwa kuwa tayari ameingia makubaliano na Manchester United na hivyo yupo tayari kudondosha saini kwa kandarasi ya miaka mitano (5) inaelezwa kuwa atakuwa akivuta mkwanja wa paundi laki 340,000 kwa wiki.
Nyota huyo wa Borussia Dortmund anajiunga Man United kwa dili la usajili la pundi milioni 110, hii ni kwa mujibu wa BILD.
Sancho kwa sasa kilichobaki ni makubaliano binafsi na Mashetani hao wekundu kabla ya kumwaga wino ili kukamilisha usajili huo.
Dortmund inatarajia kuingiza faida kubwa kutokana na mauzo ya winga huyo kwakuwa ili msajili kwa dau la paundi milioni 8 mwaka 2017 akitokea Manchester City na wao sasa baada ya miaka mitatu wanamuuza kwa paundi milioni 110.
Majadiliano yanaelekea kufikia ukingoni na yanatarajiwa kufikia tamati wiki ijayo. Baada ya usajili wa paundi milioni 110 wa nyota huyo mwenye umri wa miaka 20, na ndiyo mchezaji aliyesajiliwa kwa bei ghali zaidi ndani ya Klabu zote England baada ya Paul Pogba kununuliwa kwa paundi milioni 89 akitokea Juventus mwaka 2016.
SOMA NA HII  JAMHURI DODOMA, JKT TANZANIA V YANGA, MAMBO YAPO NAMNA HII