Home Uncategorized WIKI YA WANANCHI YAPAMBA MOTO, TIMU YA BURUNDI NDANI YA BONGO

WIKI YA WANANCHI YAPAMBA MOTO, TIMU YA BURUNDI NDANI YA BONGO

 

KLABU ya Yanga, imeanza sherehe zao kuelekea kilele cha Wiki ya Mwananchi ambapo uzinduzi ulifanyika rasmi jijini Dodoma Agosti 22 na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa klabu hiyo na wanachama wao.

Kilele cha Wiki ya Wananchi kinatarajiwa kuwa Agosti 30, Uwanja wa Mkapa na inatarajiwa kucheza mchezo wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya  Eaglenor ya Burundi.


Katika uzinduzi huo, yalifanyika maandamano ya amani kuanzia Uwanja wa Jamhuri na kumalizikia Viwanja vya Mashujaa jijini humo.Lengo la maandamano hayo ni kuwa karibu na wananchi pamoja na kusaidia jamii katika uchangiaji wa damu.


Zoezi la kuchangia damu lilifanyika katika Viwanja vya Mashujaa likiongozwa na baadhi ya viongozi wa klabu hiyo akiwemo Mwenyekiti wa Yanga, Mshindo Msola, Mwenyekiti wa Kamati ya Hamasa, Suma Mwaitenda, Ofisa Mhamasishaji, Antonio Nugaz na wengineo.

 

Katika hatua nyingine, Yanga inatarajiwa kupambana na Coastal Union katika mchezo maalum wa Kombe la GSM utakaochezwa Agosti 26, mwaka huu kwenye Uwanja wa Mkwakwani, Tanga.

 

Katibu Mkuu wa Coastal Union, Rashid Mgweno, alisema: “Mchezo huu wa GSM Cup umetokana na makubaliano ya mauzo ya mchezaji, Bakari Nondo Mwamnyeto ambao unaweza kuwa endelevu kwa miaka ijayo na itaweza kushirikisha timu mbalimbali.”

SOMA NA HII  MATTY LONGSTAFF AWEKWA KWENYE ANGA ZA UDINESE