Home Uncategorized YONDANI NA YANGA MAMBO BADO

YONDANI NA YANGA MAMBO BADO


KELVIN Yondani, beki kisiki ndani ya Klabu ya Yanga iliyo kwenye mchakato wa mabadiliko kwa sasa inaelezwa kuwa amegoma kusaini dili jipya la kuendelea kuitumikia timu hiyo.

Habari kutoka ndani ya Yanga zinaeleza kuwa nyota huyo ameahidiwa kulipwa mshahara ila hatapewa mkwanja wa usajili jambo ambalo Yondani kagoma.

“Yanga wamemuambia kwamba wanahitaji huduma yake ili asaini mkataba mwingine, ila wamemwabia kwamba hatapewa mkwanja wa usajili jambo ambalo Yondani hata haelewi na amegoma kusaini.

“Bado wapo kwenye mazungumzo ili kumshawishi beki huyo wamalizane naye kwani amekuwa na mchango mkubwa ndani ya kikosi hasa kwa kuunganisha wachezaji wenzake na hata ukongwe wake ni dawa,” ilieleza taarifa hiyo.

Mkataba wa Yondani umeshafika tamati na taarifa iliyotolewa na Yanga ilikuwa kwenye mazungumzo naye ili aongeze mkataba.

Mchezaji mwingine ambaye Yanga ipo naye kwenye mazungumzo ya kuongeza mkataba naye ni Juma Abdul, nahodha msaidizi mwenye pasi sita za mabao ndani ya ligi msimu wa 2019/20.

SOMA NA HII  AZAM FC WABABE WA WACONGO KAZINI LEO FAINALI