Home Uncategorized AZAM FC KITAMBO WALITIA TIMU AL AHLY, CORONA YATIBUA WAO KUTUA REAL...

AZAM FC KITAMBO WALITIA TIMU AL AHLY, CORONA YATIBUA WAO KUTUA REAL MADRID


OFISA Habari wa Azam FC, Zakaria Thabit amesema kuwa Azam FC Uongozi wa timu hiyo ulishatia timu kitambo makao makuu ya Al Ahly na Zamalek kwa ajili ya kujifunza huku ziara nyingine ya kwenda Real Madrid ikikwama kutokana na janga la Corona.

Thabit amesema:” Januari mwaka huu, 2020. Mtendaji Mkuu wa Azam FC, (CEO), Abdulkarim Amin alienda jijini Cairo Misri kufanya ziara kwenye vilabu vya Al Ahly na Zamalek.


“Hivi ndivyo vilabu viwili vikubwa zaidi barani Afrika na mwaka 2000, Shirikisho la Soka Duniani, FIFA, lilivitangaza kwamba ni vilabu bora vya karne ya 20.

“Katika ziara yake, Popat alijifunza mambo mengi juu ya namna ya kuendesha utawala na biashara ya soka, kuiweka klabu karibu na mashabiki pamoja kuboresha idara ya habari kama kioo cha klabu na chanzo cha mapato.

“Al Ahly ni klabu yenye idara kubwa sana ya habari ambayo inamiliki chaneli yake ya luninga inayoitwa Al Ahly TV ambayo huonesha mechi za kirafiki za klabu hiyo, mechi za vijana na mechi za michezo mingine kwa sababu klabu yao ya Sports Club, wana michezo mingi hai.

“Aliporudi nyumbani ndipo akaanzisha idara ya habari ya klabu.Mwaka huu alitakiwa aende klabuni Real Madrid kujifunza mambo mengine mengi kuhusu soka ili kuleta ufanisi kwenye klabu yetu.

“Lakini bahati mbaya ndiyo ukazuka ugonjwa wa Corona uliosimamisha mambo mengi duniani.
Lakini Inshallah, mwakani inawezekana ziara hii ikafanikiwa.

“Hata hivyo, baadaye mwaka huu ataenda Afrika Kusini kwenye vilabu vya Kaizer Chiefs, Mamelodi Sundowns na Orlando Pirates katika muendelezo wa ziara za kujifunza namna bora ya kukuza klabu.”

SOMA NA HII  HIYO VITA YA MTIBWA SUGAR V YANGA NI BALAA