Home Uncategorized MTANZANIA CHEKA ASHINDA UBINGWA KWA POINT MBELE YA MMALAWI

MTANZANIA CHEKA ASHINDA UBINGWA KWA POINT MBELE YA MMALAWI


 BONDIA wa Tanzania, Cosmas Cheka, ameshinda pambano dhidi ya Mmalawi, Hannock Phiri, lililofanyika Uwanja wa Jamhuri, Morogoro, usiku wa kuamkia leo Septemba 14, 2020.

Mabondia hao walipigana kwa uzito wa Light kuwania UBO International Title ambapo pambano hilo lilikuwa la round 12.

Kwa uamuzi wa majaji, ameonekana kushinda japo mpinzani wake ameonekana kutokubaliana na uamuzi huo wa kupoteza pigano hilo.

Mbali na hayo, Cheka amesema kuwa kama mpinzani wake hajaridhika, arudie pambano na kwamba yeye yuko tayari kumfuata Malawi.

Katika mapambano ya utangulizi, Mwanadada Zulfa Macho, mtoto wa Yusuph Macho alishinda kwa knock-out kwenye raundi ya kwanza kwenye pambano dhidi ya Mmalawi, Ndau Chilimba.

SOMA NA HII  HAJI MANARA AWAONEA WIVU YANGA