Home Uncategorized NAMUNGO HESABU ZAO NDANI YA LIGI KUU BARA

NAMUNGO HESABU ZAO NDANI YA LIGI KUU BARA

 

HITIMANA Thiery, Kocha Mkuu wa Namungo FC amesema kuwa kwa sasa hesabu zake ni Kwenye mchezo wake wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Coastal Union utakaopigwa Septemba 6.

Mchezo huo utakuwa ni wa Kwanza kwa Namungo FC kwa msimu mpya wa 2020/21 ambao ulifunguliwa Agosti 30 kwa mchezo wa Ngao ya Jamii kati ya Simba na Namungo FC uliopigwa Uwanja wa Sheikh Amri Abeid,Arusha.

Mchezo huo Namungo FC ilipoteza kwa kufungwa mabao 2-0 na yalijazwa kimiani na John Bocco kwa penalti dakika ya 7 na Bernard Morrison dakika ya 60.

Akizungumza na Saleh Jembe, Thiery amesema kuwa kupoteza mchezo wao uliopita ni kutokana na makosa waliyofanya hivyo watarekebisha ili kuwa imara zaidi.

“Mchezo wetu wa Ngao ya Jamii umeshapita hatuwezi kubadili matokeo.  Tunachofanya kwa sasa ni kuongeza nguvu kuelekea mechi zetu za Ligi Kuu Bara hakuna jambo jingine, ” amesema.

Msimu wa 2019/20, Namungo FC iliamaliza ikiwa nafasi ya nne kibindoni ilikuwa na pointi 64 baada ya kucheza mechi 38.

SOMA NA HII  SVEN: WACHEZAJI WAPO VIZURI, BADO TUNAENDELEA KUWAREJESHA KWENYE UBORA