Home Uncategorized POGBA AMERUDI ILA BADO HAJAWA FITI

POGBA AMERUDI ILA BADO HAJAWA FITI

 


KIUNGO wa Manchester United, Paul Pogba amerejea katika mazoezi ya kikosi hicho baada ya kuwa nje, lakini kuna uwezekano mkubwa wa kutocheza mchezo wa awali dhidi ya Crystal Palace.

 

Manchester United itavaana na Crystal Palace, Septemba 19, mwaka huu kwenye Uwanja wa Old Trafford ikiwa ni mchezo wa kwanza msimu huu ndani ya Premier.

 

Pogba hakuwa sehemu ya kikosi hicho ambacho kilikuwa kinaendelea na mazoezi na hii ni kutokana na kupata maambukizi ya Virusi vya Corona. 


Kocha wa Manchester United, Ole Gunnar Solskjaer amesema kuwa, Pogba amerejea kwenye mazoezi lakini ufiti wa asilimia 100 katika mechi ijayo hana uhakika kwenye hilo.


Solskjaer amesema: “Paul alifanya mazoezi ya awali, lakini baadaye akawa nje kutokana na kupata Virusi vya Corona hivyo akawa nje ya timu.


“Ninaamini atakuwa fiti tu tena kwa haraka sababu alianza kufanya mazoezi binafsi kwa bidii akitokea karantini na sasa amejiunga na timu.

 

“Matumaini yangu ni kuona wiki ijayo anakuwa fiti kwa ajili ya kupambana ingawa kwenye hilo sina uhakika, kwani anaweza kukosa ule mchezo wa kwanza,” 


Msimu uliopita, Pogba alicheza mechi 22 tu kutokana na kupata majeraha ya enka huku akicheza mechi 14 baada ya kutoka kwenye janga la Virusi vya Corona.

SOMA NA HII  MORRISON AKINUKISHA TENA YANGA ADAI HAJALIPWA MKWANJA WAKE, UONGOZI WA YANGA WAFUNGUKA