Home Uncategorized SIMBA :MSIMU HUU NI MGUMU KWETU

SIMBA :MSIMU HUU NI MGUMU KWETU

 MSHAMBULIAJI na nahodha wa Simba, John Bocco amesema kuwa huu utakuwa msimu mgumu kwao kwenye Ligi Kuu Bara kutokana na kila timu kuwapania lakini watapambana kuhakikisha wanapata matokeo mazuri.

 

Simba ni mabingwa watetezi wa kombe la ligi baada ya kulitwaa taji hilo msimu wa 2019/20 wakiwa na pointi 88 kibindoni baada ya kucheza mechi 38 wanakibarua ikiwa ni mara yao ya tatu mfululizo.

 

Simba katika mechi ya kwanza msimu huu ilifanikiwa kupata ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Ihefu Uwanja wa Sokoine ikabanwa mbavu na Mtibwa Sugar kwenye sare ya kufungana bao 1-1 kisha ikashinda mabao 4-0 mbele ya Biashara United Uwanja wa Mkapa.

 

 Bocco amesema kuwa kitendo cha wao kuchukua ubingwa wa ligi mara tatu mfululizo ndiyo kumesababisha wapaniwe na kila timu.

 

 

“Tuna kazi kubwa ya kufanya pia kwa msimu huu wa 2020/21 hasa ukizingatia sisi ni mabingwa watetezi na kila timu ambayo tunakutana nayo inahitaji ushindi kama ambavyo nasi tunahitaji pia.

 

“Hivyo, tunajipanga kuhakikisha tunapambana ili tupate matokeo mazuri, tunafahamu timu pinzani wanatupania lakini hiyo haitufanyi tupate hofu na badala yake kila mchezaji anajituma na kutimiza majukumu yake ingawa tunafahamu kuwa upinzani utakuwa mgumu,” amesema Bocco.


Kwa sasa Simba inajiandaa na mchezo wake wa pili ikiwa nyumbani dhidi ya Gwambina FC utakaopigwa Septemba 26 Uwanja wa Mkapa majira ya saa 1:00 usiku.

SOMA NA HII  MUONEKANO WA UKURASA WA MBELE GAZETI LA CHAMPIONI IJUMAA