Home Uncategorized YANGA KUONGEZA MASHINE MPYA NNE ZA KAZI KWA AJILI YA MTIBWA SUGAR

YANGA KUONGEZA MASHINE MPYA NNE ZA KAZI KWA AJILI YA MTIBWA SUGAR

 


KIKOSI cha Yanga kinachonolewa na Kocha Mkuu, Zlatko Krmpotic kinatarajia kuanza safari leo kueleleka Morogoro kwa ajili ya mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Mtibwa Sugar utakaopigwa Uwanja wa Jamhuri, Septemba 27, Jumapili.


Kwa mujibu wa Meneja wa Yanga, Hafidh Saleh kikosi kitaondoka na wachezaji 25 waliosajiliwa na Yanga ikiwa ni pamoja na wale wanne ambao walikosa mchezo wa ligi dhidi ya Kagera Sugar uliochezwa Uwanja wa Kaitaba na Yanga kushinda bao 1-0.

Wachezaji hao ambao wataunganishwa ni pamoja na Abdalah Shaibu,’Ninja’, Paul Godfrey,’Boxer’ Juma Mahadhi na Farouk Shikalo.

“Tunakwenda na wachezaji wetu wote tuliowasajili 25 kwa gari na tutapata muda wa kufanya mazoezi ili kujiweka sawa, lengo ni kuona kwamba tunapata pointi tatu muhimu,” amesema.


Mtibwa Sugar inawakaribisha Yanga kwa mara ya kwanza ndani ya msimu wa 2020/21 ikiwa imetoka kushinda bao 1-0 mbele ya Ihefu mchezo uliochezwa Uwanja wa Sokoine.


Yanga pia inawafuata Mtibwa ikiwa imetoka kushinda bao 1-0 mbele ya Kagera Sugar hivyo mchezo unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa kwa timu zote mbili kusaka pointi tatu.

SOMA NA HII  DUCHU WA LIPULI AMALIZANA NA SIMBA, AJIFUNGA MIAKA MIWILI