Home Uncategorized YANGA YAZIFUATA POINTI TATU ZA MTIBWA SUGAR LEO, MORO

YANGA YAZIFUATA POINTI TATU ZA MTIBWA SUGAR LEO, MORO


 UONGOZI wa Yanga umesema kuwa upo tayari kwa ajili ya mchezo wao wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Mtibwa Sugar unaotarajiwa kuchezwa Septemba 27, Uwanja wa Jamhuri, Morogoro.

Akizungumza na Saleh Jembe, Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Fredrick Mwakalebela amesema kuwa kikosi kipo tayari kwa ajili ya mchezo huo kwa kuwa wamejiandaa kushinda.

“Leo kikosi kimeanza safari kuelekea Morogoro, hakuna majeruhi mpya ndani ya kikosi kwa sasa kwa taarifa ambazo zimetoka benchi la ufundi.

“Mapinduzi Balama yeye kwa sasa anaendelea vizuri hivyo tunaona kwamba kila kitu kipo sawa na tunachohitaji ni pointi tatu muhimu,” amesema.


Yanga itashuka uwanjani ikiwa na kumbukumbu ya kushinda kwa bao 1-0 mbele ya Kagera Sugar inakutana na Mtibwa Sugar ambayo imetoka kushinda kwa bao 1-0 mbele ya Ihefu FC.

SOMA NA HII  NYOTA WA YANGA AIBUKIA ZESCO UNITED