Home Uncategorized HIKI NDICHO WANACHOKITAKA

HIKI NDICHO WANACHOKITAKA


Anaandika Saleh Jemba


Bahati MBAYA, mchezo wa soka huwa hautoi furaha ya milele kwa UPANDE mmoja.


Tunaweza kujifunza msimu huu wa 2020/21 ikatusaidia kuongeza ufahamu kuhusiana na soka hata kama unaipenda vipi timu yako…


Ilikuwa vigumu kuamini Yanga ingeweza kuhimili mikiki hadi mechi angalau ya saba ikiwa imeshinda sita na sare moja kwa kuwa ilibadili nusu ya kikosi na ikaanza kwa kusua.


Azam FC walianza vema zaidi, wamepoteza kabla ya Yanga na Yanga wakishinda watakuwa juu yao. Simba yenye kikosi bora kwa kuchukua mara tatu mfululizo, ndani ya mechi 7, wamedondosha pointi 8 huku wakipoteza pointi 6 katika mechi 2.


Hii inatoa funzo soka halitakupa kila unachotaka na hupaswi kuwa mwendawazimu au kuehuka au kugombana na watu au kutukana hovyo kwa kuwa mchezo wa soka unapaswa ufurahiwe na wanaouelewa.


Angalia mwendo wa Yanga sasa, ni bora kabisa. Lakini hauwapi uhakika pia wa kila kitu, siku moja unaweza kubadilika na kuwa usiotarajiwa.


Soka mchezo wa kiungwana kwa maana ya kukubaliana na uhalisia na si uadui na chuki.


Tujifunze kukubaliana na nature ya mchezo wenyewe. Ukifungwa kubali, timu isipokuwa na performance nzuri tafakari, acha kukasirika na kulalama au kuwasingizia watu MANENO YA UONGO….


UKUMBUKE soka ni MGAWANYO WA FURAHA, leo UNASHINDA tu, kesho UTASHINDWA na yote yapokeee na kama unaona haiwezekani, basi CHAGUA MCHEZO MWINGINE WA KUUSHANGILIA….


SOMA NA HII  MESSI APATWA KIGUGUMIZI KUMZUNGUMZIA ANTONIE