Home Uncategorized MKUDE AGANDA NA KITAMBAA CHA UNAHODHA DAKIKA 90

MKUDE AGANDA NA KITAMBAA CHA UNAHODHA DAKIKA 90

 


JONAS Mkude, kiungo mkabaji ndani ya Simba ambaye ana uhakika wa namba kikosi cha kwanza Oktoba 26 wakati timu yake ikipewa dozi ya bao 1-0 dhidi ya Ruvu Shooting alivaa kitambaa cha unahodha kwa muda wa dakika 90 licha ya kuwepo kwa nahodha msaidizi Mohamed Hussein, ‘Tshabalala’ ndani ya kikosi cha kwanza.


Licha ya nahodha mkuu wa Simba, John Bocco kuingia ndani akitokea benchi na kutumia dakika 24 huku akikosa penalti moja dakika ya 79 bado Mkude alivaa kitambaa hicho jambo lililoibua maswali kwa wadau kuhusu nafasi ya Bocco na Tshabalala ndani ya Simba. 

Mkude ambaye aliwahi kuwa nahodha kamili wa kikosi hicho kabla ya kuvuliwa kitambaa chake aliyeyusha dakika 90 ndani ya uwanja wa Uhuru akiwa amevaa kitambaa hicho licha ya Bocco kuingia kuongeza nguvu kwenye kikosi hicho ambacho kimepoteza mechi mbili mfululizo.

Kilianza kuchapwa bao 1-0 dhidi ya Tanzania Prisons na kikakubali kuchapwa bao 1-0 dhidi ya Ruvu Shooting na kuwafanya wayeyushe pointi sita ndani ya dakika 180.

Kuhusu suala hilo nahodha Bocco amesema kuwa hakuwa akiwaza juu ya kitambaa cha unahodha zaidi ya kufikiria namna atakayoweza kutimiza majukumu yake katika kuipa Simba ushindi.

“Hakuna ambaye alikuwa anawaza kuhusu kitambaa cha unahodha, wote tulikuwa tunafikira namna gani tunaweza kuipa ushindi timu hivyo hakuna jambo ambalo linaendelea kwa sasa tupo vizuri,” amesema.
SOMA NA HII  KWA KUNDI HILI LA YANGA KWELI MBOGA MOTO UGALI MOTO